Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Wachezaji wa Harambee Stars waahidiwa kitita cha pesa

media Sebastian Migne (Kushoto) kocha mpya wa Harambee Stars, akitambulishwa rasmi na rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Nick Mwendwa (Katikati) jijini Nairobi Mei 03 2018 FKF

Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF), limetangaza mfumo utakaotumiwa kuwalipa marupurupu wachezaji wa timu ya taifa Harambee Stars watakaoshiriki katika fainali ya bara Afrika nchini Misri, kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Rais wa FKF Nick Mwendwa, amesema kuwa wachezaji wote 23 na kocha Sebastian Migne watalipwa Shilingi za Kenya 750,000 sawa na Dola 7,500 kipindi chota watakachokuwa nchini Misri.

Mbali na malipo hayo, kila mchezaji atalipwa Dola 2,500 sawa na Shilingi 250,000 kwa kila mechi watakayoshinda.

Serikali ya Kenya imetenga bajeti ya Shilingi za nchi hiyo zaidi ya Milioni 200 kuisaidia Harambee Stars katika mashindano hayo.

Droo ya fainali hii itafanyika siku ya Ijumaa jijini Cairo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana