Pata taarifa kuu
AFCON 2019-CAF-SOKA-MISRI

Mataifa 24 yaliyofuzu kucheza fainali ya AFCON 2019

Mataifa 24 yatakayoshiriki katika fainali ya 32 ya Afrika itakayofanyika nchini Misri kati ya tarehe 21 mwezi Juni hadi 19 Julai nchini Misri, zimefahamika, baada ya kumalizika kwa michuano ya kufuzu, Jumapili iliyopita.

Kombe la bara Afrika
Kombe la bara Afrika SuperSport
Matangazo ya kibiashara

Michuano hii kwa mara ya kwanza, itashirikisha mataifa 24 kutoka 16 kama ambavyo ilivyokuwa miaka iliyopita.

Madagascar na Burundi zimeandikisha historia baada ya kufuzu katika fainali hiyo kwa mara ya kwanza.

Tanzania nayo imerejea katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya miaka 39, baada ya kupata ushindi dhidi ya Uganda mabao 3-0 jijini Dar es salaam.

Mara ya mwisho kwa Tanzania kushiriki katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria.

Mataifa yaliyofuzu ni pamoja na Senegal, Madagascar, Morocco, Cameroon, Mali, Burundi, Algeria, Benin, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana na Kenya.

Mengine ni pamoja na Zimbabwe, DR Congo, Guinea, Ivory Coast, Angola, Mauritania, Tunisia, Misri, Guinea-Bissau, Namibia, Uganda na Tanzania.

Droo ya hatua ya makundi kutafuta taji hili, itafanyika tarehe 12 mwezi Aprili mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.