Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Tanzania yarejea kwenye michuano ya AFCON baada ya miaka 38

media Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Machi 24 2019 Tanfootbal

Tanzania imeandikisha historia baada ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38, kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya kufuzu ya  kundi L, iliyochezwa Jumapili jioni jijini Dar es salaam.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na  wachezaji Simon Msuva katika dakika ya 21 ya mechi hiyo, huku beki  Erasto Nyoni akifunga bao la pili  kupitia mkwaju wa penalti.

Agrey Moris naye alihakikisha Tanzania inapata ushindi wa kuridhisha, baada ya kuifunga Taifa Stars bao la tatu katika dakika 57, kupitia shambulizi la kichwa lililomwacha kipa wa Uganda Dennis Onyango akishindwa kuokoa shambulizi hili.

Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuzu katika fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria na imefuzu nchini Misri, chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.

Wachezaji wote wa Taifa Stars waliocheza mechi za hatua ya makundi kufuzu kuelekea Misri,  walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho nchi yao iliposhiriki katika michuano ya bara Afrika.

Licha ya kufungwa, Uganda imefuzu katika fainali hiyo ikiwa inaongoza kundi hilo kwa alama 13, huku Tanzania ikiwa ya pili kwa alama nane.

Kutofungana kwa  Cape Verde na Lesotho, jijini Praia pia kumeisaidia Tanzania kufuzu.

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana