Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Vijana barani Afrika wapambana kufuzu fainali za Afrika mwezi Novemba

media Moajapo ya mechi ya vijana mwaka 2019 www.cafonline.com

Emerging Stars imejikwaa baada ya kufungwa na Sudan mabao 2-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa ugenini katika mchuano wa hatua ya pili, kufuzu kicheza fainali ya vijana wasiozidi miaka 23 barani Afrika, itakayofanyika mwezi Novemba nchini Misri.

Waleed Hamid ndiye aliyeifungia Sudan mabao yote mawili, bao la kwanza likitikisa nyavu ya Kenya katika dakika 33 huku bao la pili na la ushindi likifungwa kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 75.

Kenya inahitaji kufunga mabao 3-0 itakapocheza na Sudan tarehe 26 mwezi Machi, katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi, ili kusinga mbele katika hatua ya tatu na ya mwisho ya kufuzu.

Matokeo mengine, DRC iliishinda Morocco mabao 2-0, Libya ikailemea Nigeria pia kwa mabao 2-0 huku Sudan Kusini na Tunisia wakishindwa kufungana.

Burundi ikicheza nyumbani dhidi ya Congo Brazaville, timu zote mbili zilimaliza mchehzo huo kwa kutofugana katika uwanja wa Mwana Mfalme Loius Rwagasore jijini Bujumbura.

Mataifa nane, yatashiriki katika fainali hiyo, huku timu zitakazomaliza katika nafasi tatu bora, zitafuzu katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Japan mwaka 2020.

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana