Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Marekani: Spika wa Baraza la Congress Nancy Pelosi atoa wito wa kuandaa mashtaka dhidi ya Trump kwa ajili ya ung'atuzi
Michezo

FC Barcelona kumkosa uwanjani Dembélé kwa siku 15

media Ousmane Dembélé, mshambuliaji wa FC Barcelona. REUTERS/Albert Gea

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembélé, anayechezea FC Barcelona katika soka ya ligi kuu ya Uhispania (La liga), hatoshiriki mechi kwa siku 15 kutokana na majeraha.

Dembélé, mwenye umri wa miaka 21, alipata majeraha hayo wakati wa mchezo baina ya Barcelona na Leganes ambapo Barcelona iliibuka na ushindi wa bao 3-1. Katika mchezo huo imethibika kwamba aliteguka fundo la mguu wa kushoto.

Dembélé atarudi uwanjani baada ya siku 15. Katika michezo 27 ya msimu huu aliyoingia dimbani Dembélé amefanikiwa kufunga magoli 13.

Mfahamu Ousmane Dembélé

Ousmane Dembélé (alizaliwa 15 Mei 1997) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anachezea klabu ya Barcelona F.C. na timu ya kitaifa ya Ufaransa.

Dembélé alianza kazi yake ya soka huko Rennes kabla ya kujiunga na klabu ya Dortmund mwaka 2016. Mwaka mmoja baadaye, alihamia Barcelona kwa ada ya awali ya € milioni 105.

Borussia Dortmund

Baada ya kushinda Vikombe 20 na kufunga magoli matano katika ngazi ya vijana, Dembélé alipandishwa kwenda ligi daraja la kwanza mwaka 2016 na klabu ya Borussia Dortmund.

Mnamo Mei 12, 2016, Dembélé alisaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund. Mnamo tarehe 14 Agosti 2016, Dembélé alianza kucheza na kushinda 2-0 dhidi ya Bayern Munich katika DFL-Supercup.

FC Barcelona

Tarehe 25 Agosti 2017, FC Barcelona ya La Liga ilitangaza kuwa wamefikia makubaliano ya kutia saini kwamba wanataka kumnunua Dembélé kwa € milioni 105 pamoja na kuongeza milioni 40 za ziada.

Ousman Dembélé alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Barcelona dhidi ya Espanyol ambapo alitokea benchi na kutoa msaada kwa Luis Suarez, Barcelona wakapata ushindi wa 4-0. Alicheza tena mechi yake ya pili dhidi ya Juventus katika klabu bingwa Ulaya. Mechi yake ya tatu ilikuwa dhidi ya Granada ambapo aliumia na kukaa nje kwa myezi minne.

Alirudi Desemba 2017 kwenye mechi dhidi ya Celta Vigo kwenye kombe la mfalme.

Bao lake la kwanza alifunga dhidi ya Chelsea kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. Bao lake la kwanza kwenye La Liga alifunga dhidi ya Celta Vigo kwenye sare ya 2-2.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana