Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Michuano ya ligi kuu kuendelea DRC

media TP Mazembe inaongoza ligi kuu ya DRC kwa alama 40. STRINGER / AFP

Mechi za ligi kuu ya soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinarejelewa tena baada ya kuahirishwa kwa sababu ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwisho wa mwezi wa Desemba mwaka 2018.

Klabu ya Groupe Bazano yenye makao yake mjini Lubumbashi, inayoshikilia nafasi ya 10 katika msururu wa ligi kuu kwa alama 13, siku ya Alhamisi itamenyana na DC Motema Pembe.

Mechi hii itachezwa katika uwanja wa Frederic Kibassa Maliba mjini Lubumbashi.

Baada ya mechi Alhamisi, Groupe Bazano itakuwa na kibarua kingine nyumbani mwishoni mwa wiki dhidi ya AS Vita Club ya Kinshasa, kabla ya kusafiri kwenda kumenyana na Maniema Union katikati ya wiki ijayo.

Mechi zingine za siku ya Alhamisi, Januari 03 2019:-

Nyuki vs Renaissance

Don Bosco vs Vita Club

Ijumaa, Januari 04 2019

Mont Bleu vs Rangers

Maniema Union vs Motema Pembe

Jumapili, Januari 06 2018

Dauphins Noirs vs Nyuki

Don Bosco vs Motema Pembe

Groupe Bazano vs Vita Club

Ligi hiyo inaongozwa na TP Mazembe ambayo ina alama 40, baada ya mechi 15, ikifuatwa na Vita Club ambayo baada ya mechi 11 ina alama 28.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana