Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/01 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/01 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Urusi: Vladimir Putin ametoa mapendekezo yake kuhusu marekebisho ya katiba (Bunge)
 • Mkurugenzi wa BBC Tony Hall atangaza kuwa atajiuzulu katika msimu huu wa Joto
Michezo

Simba SC yarejea katika hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa Afrika

media Klabu bingwa Afrika CAF Online

Klabu ya soka ya Simba SC kutoka Tanzania, imerejea katika hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15.

Hatua hii ilikuja, baada ya klabu hiyo kuiondoa Nkana ya Zambia kwa kuwafunga mabao 3-1 katika mechi ya mzunguko wa pili iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaam.

Simba ilijihakikishia nafasi hiyo, katika dakika za lala salama baada ya Mzambia Clatous Chama, kuifungia klabu yake bao muhimu na kumaliza mchuano huo kwa ushindi wa mabao 4-3.

Mechi ya kwanza wiki iliyopita mjini Kitwe, Nkana walipata ushindi wa mabao 2-1.

Klabu nyingine kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zilizofuzu katika hatua hii uya makundi ni pamoja na mabingwa wa mwaka 2015, TP Mazembe kutoka DRC, walioishinda ZESCO United ya Zambia mabao 2-1.

AS Vita Club, pia imefuzu baada ya kuishinda Bantu FC ya Lesotho mabao 5-2 baada ya mechi za nyumbani na ugenini.

Droo ya hatua ya makundi inatarajiwa kutolewa tarehe 28 mwezi Desemba.

Klabu zilizofuzu ni pamoja na: Al-Ahly, Wydad Casablanca, Esperance de Tunis, Mamelodi Sundowns, Horoya, Club Africain, ASEC Mimosas, Orlando Pirates, CS Constantine, JS Saoura, Ismaily, Lobi Stars, FC Platinum.

Wakati uo huo, klabu 15 ambazo zitamenyana katika hatua ya mwondoano kutafuta timu zitakazofuzu katika hatua ya makundi, zimefahamika.

Hatua hii inakutanisha klabu zilizopata ushindi katika mechi za Shirikisho na zile zilizofungwa katika michuano ya klabu bingwa.

Miongoni mwa klabu hizo ni pamoja na: ZESCO United, Al-Hilal, Gor Mahia, Nkana, Vipers, Zamalek, KCCA na Mukura Victory Sports.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana