Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Kenya yachukuwa nafasi ya Sierra Leone katika fainali za bara Afrika 2019

media Kenya ikikabiliana na Zanzibar katika fainali ambayo Harambee Stars ilishinda kwa mabao 4-3 katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos cecafafootball.org

Kenya, imefuzu katika fainali za bara Afrika katika mchezo wa soka mwaka 2019. Hili limetangazwa rasmi na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, baada ya kuiondoa Sierra Leone, kwenye michuano ya kufuzu kuelekea katika michuano hiyo mikubwa.

Hatua hii imechukuliwa kwa sababu, Sierra Leone imefungiwa na Shirikisho la soka duniani FIFA, baada ya serikali kuingia masuala ya soka nchini humo, kinyume na kanuni za mchezo huo.

Wakenya wamefurahishwa na tangazo hili la CAF, huku rais Uhuru Kenyatta akisema kuwa, ni hatua nzuri sana kwa mchezo wa soka nchini humo.

Mara ya mwisho kwa Kenya, kushiriki katika michuano hii ya bara Afrika, ilikuwa ni mwaka 2004 nchini Tunisia.

Kwa mara ya kwanza, mataufa 24 yashiriki katika michuano hiyo.

Kuelekea AFCON 2019, haijafahamika mwenyeji wa michuano hii baada ya CAF, kuiponya Cameroon haki za kuwa mwenyeji kwa sababu ya maandalizi mabaya likiwemo suala tata la usalama.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana