Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Nigeria na Afrika Kusini kuchuana katika fainali ya wanawake

media Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon http://www.cafonline.com/

Nigeria na Afrika Kusini, zitamenyana kuanzia saa moja jioni saa za Afrika Mashariki katika fainali ya kuwania taji la bara Afrika kwa upande wa wanawake.

Mechi inachezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Accra jijini Ghana. Mwamuzi wa mchuano huu ni Gladys Lengwe kutoka Zambia.

Nigeria, ambao ni mabingwa watetezi, walifuzu katika hatua ya fainali baada ya kuishinda Cameroon kwa mabao 4-2, katika mechi ya nusu fainali, huku Afrika Kusini wakiishinda Mali mabao 2-0.

Siku ya Ijumaa, Cameroon iliishinda Mali mabao 4-2 katika mechi muhimu ya kumtafuta mshindi wa tatu.

Mataifa mengine yaliyoshiriki katika michuano hii ni pamoja na wenyeji Ghana, Algeria na Equitorial Guinea.

Nigeria imeshinda taji hili mara 10, mwisho ilikuwa ni mwaka 2016. Afrika Kusini haijawahi kushinda taji hili lakini imefika  fainali mara nne, mwaka 1995, 2000, 2008 na 2012.

Nigeria, Cameroon na Afrika Kusini, zimefuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia mwaka 2019 jijini Paris nchini Ufaransa.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana