Pata taarifa kuu
AFCON 2019-AFRIKA-KENYA

Kenya yafuzu AFCON 2019, Sierra Leone yaondolewa katika mechi za kufuzu

Timu ya taifa ya soka Kenya, Harambee Stars, imefuzu katika fainali ya mataifa bingwa mwaka 2019.

Wachezaji wa Harambee Stars
Wachezaji wa Harambee Stars Goal.com
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya uamuzi wa Kamati kuu ya CAF, kuamua kuiondoa Sierra Leone katika michuano ya kufuzu,baada ya kufungiwa na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Hii inaamanisha kuwa Kenya ambayo ipo katika kundi F, pamoja na Ghana na Ethiopia, itakuwa miongoni mwa timu mbili zitakazofuzu, hata iwapo itashindwa katika mechi yake ya mwisho ya kundi hilo mwezi Machi mwaka 2019.

Harambee Stars inaongoza kundi hilo kwa alama saba, mbele ya Ghana ambayo ina sita.

Mara ya mwisho kwa Kenya kucheza katika fainali ya kombe la Afrika likuwa ni miaka 15 iliyopita, nchini Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.