Pata taarifa kuu
TANZANIA-LESOTHO-AFCON

Tanzania kuvunja 'mwiko' uliodumu kwa miaka 38?

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo inashuka katika Uwanja wa Taifa Mjini Maseru kuchuana na Lesotho katiuka mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Afrika mwakani.

Emmanuel Amunike, ananuia kuipeleka Tanzania katika fainali za Afrika baada ya miaka 38
Emmanuel Amunike, ananuia kuipeleka Tanzania katika fainali za Afrika baada ya miaka 38 FIFA.COM
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ni muhimu kwa Tanzania ambayo inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kujikatia tiketi ya kushiriki fainali hizo, mara ya mwisho tanzania kushiriki fainali za Afrika ni 1980, fainali zilizofanyika nchini Nigeria.

Mashabiki mbalimbali wa Tanzania wamemiminika Mji Maseru kushuhudia mchezo huo, wakiongozwa na Waziri wa Habari na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe.

Tayari Uganda imemaliza ya kwanz akatika Kundi L na Tanzania yenye alama tano, inahitaji ushindi ili kujitwalia nafasi ya pili , itakayoiwezesha kufuzu fainali hizo.

Kocha wa Stars, Mnigeria, Emmanuel Amunike amenukuliwa na vyombo vya habari vya Tanzania akisema wachezaji wa Stars wana kila sababu ya kuandika historia kwa taifa lao.

Mwandishi wa Michezo wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka anasema ikiwa Tanzani itapata tiketi ya kushiriki fainali hizo, itakuwa fursa muhimu kwa wachezaji wa Tanzania kuonekana katika anga za kimataifa.

Watanzania wengi wamemiminika mitandaoni kuitakia kheri Taifa Stars, lakini swali linabaki itavunja mwiko uliodumu kwa miaka 38.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.