Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Droo ya michuano ya kutafuta ubingwa yaahirishwa

media Rais wa CAF Ahmad. MOHAMED EL-SHAHED / AFP

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limesema limeahirisha droo ya michuano ya kutafuta ubingwa, klabu bingwa na Shirikisho msimu 2019 kwa sababu maalum.

Droo hiyo ilitarajiwa kufanyika mjini Rabat nchini Morocco, Jumapili iliyopita.

Duru zinasema kuwa droo hiyo iliahirishwa kwa sababu klabu za Morocco zilitaka kuleta mkanganyiko kuhusu namna droo hiyo itakavyokuwa, kwa timu zake zinazocheza katika michuano ya kuwania taji la Shirikisho.

Klabu ya Hassania Agadir, Renaissance Berkane au Wydad Fes zote zinaelezwa kuwa zimefuzu kucheza fainali ya Shirikisho lakini pia iwapo Raja Casablanca itashinda fainali ya mwaka huu ya taji la Shirikisho, itafuzu pia.

Casabalanca inacheza nyumbani na ugenini dhidi ya AS Vita Club ya DRC, katika fainali hiyo.

Kanuni za CAF, haziruhusu klabu tatu kucheza katika mashindano ya kuwania taji moja, na iwapo Raja Casablanca watashinda mechi hiyo, klabu ya Hassania itabidi iondoke kwenye mashindano hayo.

Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuanza tarehe 27 mwezi Novemba na kumalizika tarehe 1 mwezi Juni mwaka 2019.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana