Pata taarifa kuu

Mmiliki wa Leicester City athibitishwa kufariki katika ajali ya Helikopta

Klabu ya Leicester City inaomboleza msiba wa mmiliki wake Vichai Srivaddhanaprabha ambaye amethibitishwa kuwa alipoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea mwishoni mwa juma.

Aliyekuwa mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha na kocha wa wakati huo Claudio Ranier baada ya kunyakua taji la EPL mwaka 2016
Aliyekuwa mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha na kocha wa wakati huo Claudio Ranier baada ya kunyakua taji la EPL mwaka 2016 Evening Standard
Matangazo ya kibiashara

Vichai Srivaddhanaprabha alikuwa sanjari na watu wengine wanne katika ndege hiyo ndogo ambayo ilianguka nje ya Uwanja wa king Power, punde  baada ya kushuhudia mchezo wa ligi Kuu mwishoni mwa Juma baina ya klabu yake na West Ham United.

Klabu yake imesema alikuwa mtu muhimu na aliyebadili fikra za mashabiki wa soka nchini Uingereza wakati alipoiongoza klabu hiyo kunyakua taji la Ligi Kuu mwaka 2016 mbele ya vigogo Chelsea, Manchester United na Liverpool.

Kifo cha Vichai Srivaddhanaprabha kimeibua hisia duniani kote ambapo mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakitoa salamu za rambirambi kwa kuweka mashada ya maua katika eneo ilipotokea ajali.

Aidha wachezaji mbalimbali wa soka na wastaafu akiwemo Didier Drogba, Wilfred Ndidi wamemiminika mitandao kutoa salamu za rambirambi kufuatia msiba huo.

Vichai Srivaddhanaprabha ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 60, licha ya alama aliyoweka kwenye mchezo wa soka anakumbukwa na raia wengi wa Thailand kwa mchango mkubwa aliotoa katika maendeleo ya taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.