Eliud Kipchoge atuzwa na Umoja wa Mataifa
Bingwa wa dunia wa mbio za Marathon nchini Kenya Eliud Kipchoge ametajwa kuwa mtu wa mwaka wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018.
Imechapishwa:
Mwanariadha huyo wa miaka 33, amepata tuzo hiyo katika Ofisi za Umoja huo jijini Nairobi, baada ya kuvunja rekodi ya mashindano ya Berin Marathon mwezi Septemba kwa muda wa saa mbili dakika moja na sekunde 39.
Aidha, Umoja wa Mataifa umempongeza kwa jitihada zake za kutoa elimu kuhusu namna ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Kipchoge, anaelezwa kuwa Mwanariadha bora duniani katika mbio za Marathon baada ya kukimbia kwa kasi na kushinda mashindano ya Berlin na London Marathon mara tatu.