Pata taarifa kuu
SOKA-ETHIOPIA-KENYA-SAINT GEORGE

Kipa wa Harambee Stars Patrick Matasi, asajiliwa na Saint George ya Ethiopia

Kipa wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Patrick Matasi, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Saint George ya Ethiopia.

Kipa wa Harambee Stars Patrcik Matasi
Kipa wa Harambee Stars Patrcik Matasi www.goal.com
Matangazo ya kibiashara

Hii imethibitishwa kupitia Gazeti la Nation Sportcan.

Kipa huyo wa klabu ya Tusker FC na Posta Rangers, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo yenye makao yake jijini Addis Ababa.

Uhamisho huu unatarajiwa kuwa mkubwa na wa kihistoria katika soka la nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

Matasi amejipatia umaarufu kwa uchezaji wake, na hajaruhusu kufungwa goli katika kampeni ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali ya mataifa bingwa barani Afrika 2019.

Mbali na Matasi, Shaffik Batambuze kutoka klabu ya Singida United nchini Tanzania, imesajiliwa na klabu ya Gor Mahia, mabingwa soka nchini Kenya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.