Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-ZAMBIA-SOKA

Guinea-Bissau yaiadhibu Zambia kwa kuifunga 2-1

Guinea-Bissau iliishangaza Zambia baada ya kuifunga mabao 2-1 jijini Bissau na kujipa matumaini ya kufuzu kucheza fainali ya bara la Afrika kwa mara ya pili.

Timu ya taifa ya Guinae-Bissau ikiwa mazoezini.
Timu ya taifa ya Guinae-Bissau ikiwa mazoezini. RFI/Marco Martins
Matangazo ya kibiashara

Zambia, ilianza vema kupitia bao la mchezaji wake Justin Shonga aliyefunga mkwaju wa Free Kick, lakini muda fupi baada ya kuanza kipindi cha pili, Stoppila Sunzu alijifunga na hivyo kuisawazishia Guinea-Bissau huku Toni Silva akiipa timu yake ushindi kwa bao la kichwa.

Kwa matokeo haya Guinea Bissau inangoza kundi lao kwa alama saba, baada ya mechi nne, huku Namibia, Msumbiji na Zambia zote zikiwa na alama nne.

Jijini Nairobi, Harambee Stars ya Kenya nayo ilipata matumaini ya kurejea katika fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 baada ya kuifinga Ethiopia mabao 3-0 katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani.

Mabao ya Harambee Stars yalitiwa kimyani na Michael Olunga , Eric Johanna na nahodha Victor Wanyama kupitia mkwaju wa penalti.

Michuano hii inaendelea kesho:-

Tanzania vs Cape Verde Island

Zimbabwe vs Congo DRC

Rwanda vs Guinea

Sudan Kusini vs Gabon

Sudan vs Senegal

Burundi vs Mali

Lesotho vs Uganda

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.