Pata taarifa kuu
AFCON 2019-AFRIKA-CAMEROON-CAF-SOKA

Kenya yahitaji alama tatu muhimu kufuzu AFCON 2019

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, inahitaji siku ya Jumapili dhidi ya Ethiopia kujiweka katika sehemu nzuri ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika AFCON mwaka 2019 nchini Cameroon.

Wachezaji wa Harambee Stars wakifanya mazoezi kabla ya kumenyana na Ethiopia jijini Nairobi Oktiba 14 2018
Wachezaji wa Harambee Stars wakifanya mazoezi kabla ya kumenyana na Ethiopia jijini Nairobi Oktiba 14 2018 www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itakuja baada ya nchi hizo mbili kukutana katika mchuano wa kwanza siku ya Jumatano jijini Addis Ababa na Kenya kulazimisha sare ya kutofungana.

Matokeo haya yameonekana kuwa mazuri kwa Kenya ambayo inaongoza kundi la F, nyuma ya Ethiopia ambayo pia ina alama nne.

Ghana ni ya tatu kwa alama tatu, huku Sierra Leone ikiwa imefungiwa na Shirikisho la soka duniani FIFA kwa muda usiojulikana kujihusisha na masuala ya soka.

Ethiopia pia ina nafasi ya kufuzu iwapo, itapata alama tatu muhimu dhidi ya Harambee Stars jijini Nairobi huku kocha wa nchi hiyo Abraham Mebartu akisema mechi hiyo itaamua hatima yao.

Kenya itamaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya Ghana, mwezi Machi mwaka 2019 huku Ethiopia ikimalizia kibarua chake dhidi ya Ghana mwezi Novemba.

Mataifa 24 yatafuzu kushiriki katika mashindano ya mwakani, kutoka mataifa 16.

Mechi hizo za kufuzu zinaendelea:-

Alhamisi Oktoba 11 2018

Congo vs Liberia

Ijumaa Oktoba 12 2018

Cameroon vs Malawi

Gabon vs Sudan Kusini

Angola vs Mauritania

Nigeria vs Libya

Guinea vs Rwanda

Cote d'Ivore vs Jamhuri ya Afrika ya Kati

Misri vs Swaziland

Cape Verde vs Tanzania

Togo vs Gambia

Mali vs Burundi

Algeria vs Benin

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.