Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
Michezo

Wachezaji 30 kuwania taji la Ballon d'Or mwaka 2018

media Taji la Ballon d'Or FABRICE COFFRINI / AFP / Getty Images

Sadio Mane kutoka Senegal na Mohammed Salah kutoka Misri, ndio wachezaji pekee kutoka barani Afrika walioteuliwa katika orodha ya wachezaji 30 wanaowania taji la Ballon d'Or mwaka 2018.

 

Hata hivyo, orodha hiyo inatawaliwa na wachezaji wengi kutoka mabingwa wa taji la klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, ambayo imewakilishwa na wachezaji wanane.

Mshambuliaji kutoka Wales ,Gareth Bale na mshambuliaji kutoka Uingereza Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji wanaowania nafasi hiyo.

Eden Hazard kutoka Chelsea, Mohammed Salah wa Liverpool na Kevin de Bruyne anayechezea klabu ya Manchester City ni miongoni mwa wachezaji 11 kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Tuzo ya Ballon d'Or ilianza kutolewa mwaka 1956 na Gazeti la michezo nchini Ufaransa France Football.

Kati ya mwaka 2010 na 2015, Ballon d'Or, ilikubaliana na Shirikisho la soka duniani FIFA ,kutoa tuzo moja iliyopewa jina la FIFA Ballon d'Or.

Cristiano Ronaldo, alishinda tuzo hii mara mbili mfululizo mwaka 2016 na 2017.

Tuzo ya mwaka huu itatolewa tarehe 3 mwezi Desemba jijini Paris.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana