Pata taarifa kuu
MCHEZO WA KIKAPU-AFRIKA-EQUITY BANK

Equity Bank Hawks yashinda ubingwa kanda ya tano mchezo wa kikapu

Klabu ya wanawake ya Equity Bank Hawks kutoka nchini Kenya ndio mabingwa wa kanda ya tano ya mashindano ya Afrika katika mchezo wa Kikapu yaliyomalizika jijini Dar es salaam nchini Tanzania mwishoni mwa juma lililopita. 

Wachezaji wa Benki ya Equity wakishiriki katika mashindano ya kanda ya tano barani Afrika jijini Dar es salaam Oktoba 5 2018
Wachezaji wa Benki ya Equity wakishiriki katika mashindano ya kanda ya tano barani Afrika jijini Dar es salaam Oktoba 5 2018 eEquityBank
Matangazo ya kibiashara

Fainali ilizikutanisha klabu zote kutoka nchini Kenya, mabingwa hao wapya na klabu ya Bandari KPA.

Mabingwa hao  walionekana imara katika idara zote na kupata ushindi wa  vikapu 24-17, 19-9 na 201-15 katika mizunguko mitatu ya mchezo huo.

Hata hivyo, KPA, walipata ushindi wa mzunguko wa mwisho wa vikapu 13-7,  lakini Equity Bank Hawks wakapata ushindi wa jumla kwa kupata vikapu 70-54.

Kocha David Maina amefurahishwa na ushindi huo na kusema, wachezaji wake walikuwa wazuri katika mechi hiyo.

“Tulikuwa bora kuwazidi  KPA katika mchuano huu, na tulikuwa imara sana, ni mafanikio makubwa kwa klabu hii iliyoanza miaka mitano iliyopita,” alisema kocha Maina.

Nayo klabu ya wanaume ya KPA, ilipoteza nafasi ya tatu, baada ya kufungwa na Energy Group ya Rwanda kwa vikapu 74-71.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.