Pata taarifa kuu
CAF-SHIRIKISHO-ENYIMBA-AS VITA

Raja Casablanca yaanza vema nusu fainali taji la Shirikisho

Abdelilah Hafidi ameipa matumaini klabu ya Raja Casablanca ya Morocco matumaini ya kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga Enyimba ya Nigeria bao 1-0, siku ya Jumatano.

Wachezaji wa Enyimba na Raja Casablanca katika mechi muhimu ya Shirikisho Oktoba 3 2018
Wachezaji wa Enyimba na Raja Casablanca katika mechi muhimu ya Shirikisho Oktoba 3 2018 www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa kati alipachika bao hilo katika dakika ya 48 ya mchuano huo, uliochezwa katika uwanja wa Aba.

Enyimba ilipoteza nafasi nyingi za kusawazisha au hata kupata ushindi.

Stanley Dimgba alipata nafasi ya kufunga kupitia mkwaju wa penalti baada ya mkwaju wa penalti kupita juu ya lango.

Mechi ya marudiano itachezwa nchini Morocco, tarehe 24 mjini Casablanca.

Nayo Vita Club ya DRC, ilijipa matumaini baada ya kulazimisha sare ya kutofungana na Al Masry ikiwa ugenini katika mjhi wa Port Said.

Mshindi wa mechi ya fainali, atajishindia Dola Milioni 1.25 na kucheza na mshindi wa taji la klabu bingwa, katika fainali ya kuwania taji la CAF Super Cup .

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.