Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Rais Biya asema Cameroon iko tayari kuandaa AFCON 2019

media Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad (Kushoto) akimkabidhi rais wa Cameroon Paul Biya (Kulia) nembo ya CAF, wakitazamwa na mchezaji wa zamani Samwel Eto'o Oktoba 2 2018 CAF_Online

Rais wa Cameroon Paul Biya amesisitiza kuwa nchi yake iko tayari kuwa mwenyeji wa mashindano ya mataifa ya bara Afrika AFCON, yatakayofanyika mwaka 2019.

Hakikisho hili, limekuja baada ya rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad kukutana na rais Biya siku ya Jumanne jijini Yaounde.

Ahmad naye amesema kuwa, CAF haina mpango wa kuondoa mashindano hayo nchini Cameroon.

“Rais Biya ametuhakikishia kuwa, atahakikisha kuwa maandalizi yote yanafanyika na kumalizika kwa wakati,” amesema Ahmad.

“Cameroon ndio inayoandaa mashindano ya AFCON, sio CAF, kwa hivyo ni wao wa kutuambia kama wako tayari au la,” ameongeza.

Rais huyo wa CAF amesisitiza kuwa kukutana kwake na rais Biya, kulilenga kundoa wasiwasi kuhusu madai ya mashindano hayo kuondolewa nchini Cameroon.

Licha ya hakikisho hili, kumeendelea kushuhudiwa wasiwasi wa usalama hasa Kaskazini Magharibi mwa hiyo lakini pia ukarabati wa viwanja kufanyika taratibu.

Mashindano ya mwaka ujao kwa mara ya kwanza, yatajumuisha nchi 24, kutafuta mshindi katika michuano hiyo mikubwa itakayochezwa kati ya mwezi Juni na Julai.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana