sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atangaza kujiuzulu
Michezo

Al-Ahly yapata matokeo mazuri, kibarua cha kuwania taji la Shirikisho kushuhudiwa

media Wachezaji wa Enyimba kutoka Nigeria wakifanya mazoezi kuelekea mechi ya Jumatano dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco. CAF Online

Mechi za nusu fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika zinachezwa siku ya Jumatano.

Enyimba ya Nigeria itafungua mchuano wa mapema, kati ya Raja Casablanca ya Morocco.

Al Masry ya Misri itakuwa nyumbani kumenyana na AS Vita Club ya DRC.

Enyimba ambayo mara ya mwisho kushiriki katika mashindano haya ilikuwa mwaka 2010 na kuondolewa katika hatua ya 16 bora.

Mwaka huu, ilifuzu katika hatua hii baada ya kuishinda Rayon Sport ya Rwanda katika hatua ya robo fainali.

Raja Casablanca nayo ilifuzu baada ya kuishinda CARA Brazaville katika mchuano wa robo fainali.

AS Vita Club inakwenda katika mechi hii ikiwa na historia ya kushiriki katika mashindano haya mara tatu, mwisho ikiwa ni mwaka 2010.

Mbali na michuano hii, siku ya Jumanne kulikuwa na mechi mbili za mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa.

Mabingwa mara nane wa taji hili, Al-Ahly ilianza vema nyumbani baada ya kuishinda ES Setif ya Algeria mabao 2-0.

Primero de Agosto ya Angola, nayo ilianza vema baada ya kuifunga Esperance de Tunis, ya Tunisia bao 1-0.

Mechi ya marudiano itachezwa tarehe 23 mwezi huu.

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana