Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Klabu Bingwa Afrika: Al-Ahly kumenyana na ES Setif

media Anice Badri, mshambuliaji wa ES Tunis, akikabiliana na beki waAl-Ahly, Sabri Raheel. STRINGER / AFP

Klabu ya Al-Ahly ya Misri, itachuana na ES Setif ya Algeria katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika. Mechi ya kwanza itachezwa tarehe 2 huku ya marudiano ikichezwa tarehe 23 mwezi Oktoba. Mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini.

Al-Ahly ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga Horoya ya Guinea mabao 4-0 baada ya mchuano wa mzunguko wa mwisho, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nayo Primero de Agosto ya Angola itapambana na Esperance de Tunis, katika mechi nyingine ya nusu fainali.

Esperance de Tunis, ilifuzu baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 baada ya mechi ya nyumbani na ugenini dhidi ya Etoile du Sahel ya Morocco, mwishoni mwa wiki.

Primero de Agosto, iliweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua hiyo kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya TP Mazembe ya DRC baada timu zote kutoka sare ya bao 1-1.

Katika taji la kuwania taji la Shirikisho, Enyimba ya Nigeria itamenyanana Raja Casablanca ya Morocco, huku Al-Masry ya Misri ikipangwa kucheza na AS Vita Ckub ya DRC.

Enyimba ilipata ushindi mkubwa baada ya kuishinda Rayon Sport ya Rwanda mabao 5-1, katika mechi yake ya nyumbani baada ya kutofungana jijini Kigali.

AS Vita Club nayo ilipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya RS Berkane baada ya kumaliza mechi yake ya ugenini.

Mechi za nusu fainali zitachezwa pia mwezi Oktoba.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana