Ligi Kuu ya Uingereza yaanza kutimua vumbi
Ligi Kuu ya soka nchini England inaanza kutimua vumbi leo ambapo mashetani wekundu Manchester United itachuana na Leicester City, majira ya saa nne kwa saa za Afrika Mashariki.
Imechapishwa:
Mabingwa mara 20, United, waanza kampeni ya kuwania taji huku meneja wake Jose Mourihno akilalama kutokana na klabu hiyo kushindwa kufanya usajili mkubwa majira haya ya joto.
Dirisha la usajili nchini humo lilitamatika jana huku Manchester United ikiwa imefanya usajili wa mchezaji mmoja, Mbrazil Fred kwa dau la Uero milioni 50.
Mechi za kesho Jumamosi
Newcastle itachuana na Tottenham Hotspurs
Fulham itachuana na Crystal Palace
Huddesfield itakabiliana na Chelsea
Bounermouth itapambana na Cardiff City
Watford itapambana na Brighton