Pata taarifa kuu
SOKA-KENYA-MICHAEL OLUNGA

Michael Olunga ahusishwa kujiunga na klabu ya Kashiwa Reysol

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Michael Olunga anatajwa kuwa njiani kujiunga na klabu ya Kashiwa Reysol ya Japan inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Michael Olunga
Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Michael Olunga www.goal.com
Matangazo ya kibiashara

Mwaka uliopita Olunga, aliitumikia Giroma ya Hispania kwa mkopo akitokea Guizhou ya China.

Ikiwa usajili huo utakamilika, Olunga atajiunga na wachezaji wengine waliokuwa wakicheza Ligi ya Hispania kuelekea nchini Japan.

Wachezaji wengine ni Andreas Iniesta, Fernando Torres na Lukas Podolski.

Kashiwa msimu uliopita ilimaliza ya 13 katika ya timu 18 katika Ligi Kuu ya soka nchini Japan

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.