Ada ya Euro milioni 71 kwa golikipa Kepa Arrizabalaga kutoka klabu ya Athletic Bilbao ya Hispania, uajili huo unakuja baada ya Chelsea kuondokewa na golikipa wake Thibaut Courtois aliyejiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa ada ya Euro milioni 35.
Aidha Chelsea imemsajili kwa mkopo wa mwaka mmoja kiungo Matteo Kovacic kutoka Real Madrid.
Awali, Liverpool ilimsajili kipa Allison kutoka AS Roma kwa ada ya Euro milioni 66.
Manchester United inahaha kusaka wachezaji nyota kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na ripoti za hivi punde zinasema inazungumza na beki wa Atletico Madrid Diego Godin ili kumpeleka Old Trafford.