Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

TP Mazembe wasubiriwa Algiers kumenyana na MC Alger

media Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea ushindi wao wakati wa michuano ya Kombe la Shirikisho, Novemba 6 Lubumbashi, DRC. STRINGER / AFP

Mabingwa wa mwaka 2010 wa taji la klabu bingwa barani Afrika TP Mazembe ya DRC, siku ya Jumanne wanatarajiwa kwenda jijini Alger nchini Algeria, kuanza maandalizi ya kumenyana na MC Alger katika mchuano muhimu wa kuwania taji la msimu huu.

Maandalizi haya ya mapema yanakuja kuelekea mechi ya Jumamosi katika uwanja wa Stade du 5 Juillet jijini Algers baada ya ushindi wa nyumbani.

TP Mazembe wakiwa nyumbani mjini Lubumbashi, waliifunga MC Alger bao 1-0, lililofungwa na Elia Meschak katika dakika ya 88 ya mchuano huo uliochezwa wiki iliyopita.

Wiki mbili baadaye, Mazembe wanatarejea kurejea tena nchini humo kumenyana na Entente Sportive de Setif tarehe 17 mwezi Agosti katika mchuano mwingine muhimu wa kufuzu katika hatua ya robo fainali kutoka kundi B.

Mazembe wanaongoza kundi hilo kwa alama 9, baada ya kushinda mechi zake zote tatu.

Wenyeji wa mchuano wa wiki hii MC Alger, wana alama nne, ES Setif ina alama tatu huku Difaa El Jadida ya Morocco ni ya mwisho kwa alama moja katika kundi hilo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana