Ufaransa yashinda kombe la dunia 2018
Timu ya Taifa ya Ufaransa Les Blue imetwaa ubingwa wa fainali za kombe la dunia baada ya kuishinda Croatia mabao 4-2. Mabao ya Ufaransa yamefungwa na Paul Pogba, Kylian Mbappe, Antoine Griezman na bao la kujifunga mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic. Mabao ya Croatia yamefungwa na Mario Mandzukic na Ivan Perisic. Tunachambua kwa kina.
Kuhusu mada hiyo hiyo