Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Tetemeko la ardhi Ufilipino: Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia watu watatu huko Mindanao
 • Pande zinazokinzana zaendelea tena na mazungumzo Jumatatu kujaribu kuiondoa Ireland ya Kaskazini katika mkwamo wa kisiasa
 • Mjumbe wa Marekani katika mazungumzo Stephen Biegun afutilia mbali msimamo wowote wa Korea Kaskazini lakini aacha mlango wazi kwa mazungumzo
Michezo

Mfahamu mwamuzi Nestor Pitana atakayechezesha fainali ya Croatia na Ufaransa

media Nestory Pitana, mwamuzi atakayechezesha fainali ya kombe la dunia baina ya Croatia na Ufaransa FIFA.COM

Je, unamfahamu mwamuzi Nestor Pitana kutoka Argentina atakayechezesha fainali ya kombe la dunia baina ya Croatia na Ufaransa.

Amekuwa mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya Fifa tangu mwaka 2010 na ni miongoni mwa waamuzi wenye uzoefu mkubwa kutoka Amerika kusini.

Mwamuzi huyu ana umri wa miaka 43 na ndiye aliyechezesha mechi ya ufunguzi wa fainali hizo, Juni 14 baina ya wenyeji Urusi na Saudi Arabia ambapo Urusi walishinda mabao 5-0.

Alichezesha fainali za kombe la dunia za vijana chini ya miaka 17 mwaka 2013 na pia alichezesha fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil, miongoni mwa mechi alizochezesha ni ile ya robo fainali baina ya Ufaransa na Ujerumani.

Ni mwamuzi wa pili kutoka Argentina kuchezesha fainali ya kombe la dunia, Horacio Elizondo muargentina mwingine alichezesha fainali ya mwaka 2006 baina ya Italia na Ufaransa.

 

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana