Pata taarifa kuu
CAF-KENYA-SOKA

CAF yawafungia waamuzi kuchezesha soka

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) imetangaza kuwafungua waamuzi kutoka mataifa mbalimbali kutokana na makosa ya kinidhamu.

Nembo za mashindano ya CAF
Nembo za mashindano ya CAF RFI Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya waamuzi waliofungiwa ni Jallow Ebrima kutoka Gambia na Yanissou Bebou kutoka Togo ambao wamefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka kumi wakati mwamuzi msaidi kutoka Kenya Aden Marwa amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka yanayosimamiwa na CAF.

Uamuzi huo umetangazwa leo baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo.

Mwezi uliopita Marwa alituhumiwa kupokea rushwa na hivyo kuondolewa katika orodha ya waamuzi wasaidizi walioteuliwa kuchezesha fainali za Kombe la dunia nchini Urusi.

Aidha waamuzi wengine wanaendelea kuchunguzwa na hatua zitachukuliwa baada ya kuitwa kwenye kamati ya nidhamu.

Orodha kamili ya waamuzi waliofungiwa

Marwa Range, mwamuzi msaidiz (Kenya) Boukari Ouedraogo, mwamuzi wa kati (Burkina Faso), Denis Dembele, mwamuzi wa kati (Cote d’Ivoire): Marius Tan, mwamuzi msaidiz (Cote d’Ivoire), Bi Valere Gouho, mwamuzi msaidizi (Cote d’Ivoire),Coulibay Abou, Rmwamuzi wa kati (Cote d’Ivoire), Jallow Ebrima, mwamuzi msaidizi (Gambia),

 

Moriba Diakite, Mwamuzi msaidiz (Mali) :

Demba Boubou, mwamuzi msaidizi kutoka Mauritania ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka mitano,Maman Raja Abba Malan Ousseini, mwamuzi msaidiz kutoka Niger ambaye pia amehukumiwa kifungo cha miaka mitano

Soma orodha kamili ya waamuzi wengine waliofungiwa na ambao wanasubiri mashauri yao kusikilizwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.