Pata taarifa kuu
CECAFA-MUSONYE-KLABU BINGWA

Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki kuanza Ijumaa nchini Tanzania

Michuano ya klabu bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, itaanza siku ya Ijumaa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye ( Wa pili kutoka kushoto) akikutana na wanahabari jijini Dar es salaam Juni 28 2018
Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye ( Wa pili kutoka kushoto) akikutana na wanahabari jijini Dar es salaam Juni 28 2018 rfi/Fredrick Nwaka
Matangazo ya kibiashara

Klabu 12 kutoka mataifa zaidi ya 10 yanatarajiwa kushiriki katika michuano hiyo mikubwa katika ukanda wa CECAFA.

Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya JKU ya Zanzibar na Vipers ya Uganda kuanzia saa nane mchana katika uwanja wa Chamazi.

Azam FC nayo itacheza na Kator FC ya Sudan Kusini.

“Tumepanga ratiba ya michuano hii ili isiingiliane na muda wa michuano ya kombe la dunia,” alisema Musonye.

"Tunaomba wadhamini wengine washirikiane na Azam na tunaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi maana wao ndio wadhamini wakubwa" aliongeza Musonye siku ya Alhamisi jijini Dar es salaam.

Mataifa yanayoshiriki katika michuano hii ni pamoja na:

Kundi A: Azam (Tanzania), Vipers (Uganda), JKU (Zanzibar), Kator FC (Sudan Kusini)

Kundi B: Rayon Sport (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Lydia Ludic (Burundi), Ports (Djibouti)

Kundi C: Yanga (Tanzania), Simba (Tanzania), St.George (Ethiopia), Dakadaha (Somalia).

Mechi zote za Kombe la Kagame zitarushwa na kituo cha Azam TV

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.