Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Senegal inahitaji sare au ushindi kufuzu hatua ya mwondoano

media Wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal wakishangilia bao dhidi ya Japan wiki iliyopita REUTERS/Marcos Brindicci

Timu ya taifa ya soka ya Senegal ina kibarua kizito dhidi ya Colombia katika mchuano wake wa mwisho wa kundi H, Alhamisi  jioni kuanzia saa 11 saa za Afrika Mashariki.

Mechi hii ni muhimu kwa Teranga Lions ambayo inahitaji sare au ushindi ili kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Senegal inakwenda katika mchuano huu ikiwa na alama nne, baada ya ushindi wa mechi moja na kutoka sare katika mchuano huo.

Colombia nayo ina alama tatu, baada ya kushinda mechi moja na kupoteza mwingine.

Mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana ilikuwa ni mwaka 2014 wakati wa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki na kutoka sare ya mabao 2-2.

Mwaka 2002, wakati wa kombe la dunia, timu hizi mbili zilikutana katika mchuano wao wa mwisho na kutoka sare ya 3-3.

Ratiba ya mechi nyingine:-

Japan vs Poland

Uingereza vs Ubelgiji

Panama vs Tunisia

Tayari Tunisia, imeondolewa katika michuano hii baada ya kupoteza michuano yake miwili, dhidi ya Ubelgiji na Uingereza.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana