Pata taarifa kuu
ARGENTINA-KOMBE LA DUNIA-FIFA

Maradona: Mheshimuni Lionel Messi

Nyota wa mchezo wa kandanda duniani, Diego Maradona amesema ataendelea  kumheshimu Lionel Messi licha ya matokeo mabaya ambayo Argentina inayapata katika fainali za Kombe la dunia.

Nyota wa Argentina, Lionel Messi.
Nyota wa Argentina, Lionel Messi. REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Maradona amecheza fainali nne za Kombe la dunia kati ya mwaka 1982 na 1994.

Messi na wenzake leo wana kibarua kigumu watakapoumana na Nigeria katika mchezo muhimu utakaoamua mabingwa hao wa mwaka 1986 watasonga mbele au la.

“Nataka kumwambia Messi, yeye hana hatia yoyote.Hana hatia yoyote.Nakupenda na kukuheshimu mara zote,”amesema Maradona ambaye alicheza fainali nne za kombe la dunia.

Nigeria inahitaaji ushindi na huku ikiomba Iceland ishindwe kupata matokeo mazuri mbele ya Croatia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.