Pata taarifa kuu
FIFA-URUSI-KOMBE LA DUNIA 2018

Kocha wa Senegal: Mabeki hawakuwa makini kuwadhiti Japan

Siku moja baada ya timu yake kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Japan kocha wa Senegal Aliou Cisse ameeleza kutoridhishwa na namna safu ya ulizi ya timu yake ilivyocheza katika mchezo huo.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal, Aliou Cisse
Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal, Aliou Cisse REUTERS/Maxim Shemetov
Matangazo ya kibiashara

Senegal ikiwa mbele kwa mabo 2-1 hadi dakika ya 75 iliruhusu bao la Keisuke Honda dakika ya 78 na kufanya matokeo kuwa sare. Senegal inahitaji ushindi au sare katika m,chezo wa mwisho wa kundi H dhidi ya Colombia ili kufuzu hatua inayofuata.

“Timu bora katika mchezo huo ilikuwa Japan na tunapaswa kukubaliana na hilo, mabeki wangu wanapaswa kuwa borta muda wote kwa kuwa ni wachezaji wakubwa na ambao wanaweza kuisaidia timu yake muda wowote uwanjani,”amesema Cisse aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Morocco kilichofika robo fainali ya michuano hiyo mwaka 2002 ilipoandaliwa kwa ushirikiano na nchi za Japan na Korea Kusini.

Mabeki wa kati wa Senegal ni Kalidou Koulibaly na Salif Sane. Senegal ina alama nnem sawa na Japan.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.