Michuano hiyo ya siku sita itaanza kesho na kufikia tamati Juni 22 mwaka huu.
Nchi zilizowasili kushiriki michuano hiyo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan na wenyeji Tanzania.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Fares magesa, amesema wanaendelea kusubiri ikiwa nchi nyingine zitawasili kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
“Changamoto za kiuchumi zimesababisha timu nyingi kushindwa kushiriki lakini nina imani hadi kufikia leo usiku tutakuwa na idadi kamili ya timu zitakazoshiriki,”
Mgeni rasmi katika michuano hiyo atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Dr Harrison Mwakyembe.
Mashindano ya vijana husaidia kukuza mpira wa kikapu katika kanda ya tano inayojumuisha mataifa 12, yakiwemo Misri, Ethiopia, Burundi na DRC ambazo hazijaleta wanamichezo wake.