Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Misri yaanza vibaya fainali za Kombe la dunia

media Jose Jiminez akishangilia baada ya kuifungia Uruguay bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Misri June 15, 2018 Sky Sports

Timu ya Taifa ya Misri 'Pharaos' imeanza vibaya fainali za Kombe la dunia nchini Urusi baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Uruguay.

 

Bao la Jose Giminez katika dakika ya 90 ya mchezo baada ya kumzidi ujanja beki Ahmed Hegazy limeiwezesha Uruguay kupata alama tatu na katika mchezo huo,Uruguay haijawahi kupoteza mchezo wowote wa ufunguzi wa fainali za Kombe la dunia.

Hata hivyo, Misri itapaswa kujilaumu kwa kupoteza nafasi za kufunga katika mchezo huo kwa kosa nafasi ya kutikisa nyavu mwanzoni mwa mchuano huo.

Mshambuliaji Luis Suarez alipoteza nafasi nne za kufunga katika mchezo huo.

Mshambuliaji Mohammed Salah hakucheza katika mchezo huo, kutokana na kutokuwa fiti baada ya kupona jeraha la bega alilopata katika mchuano wa fainali ya Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi uliopita.

Matokeo haya yana maana kwamba Urusi inashika nafasi ya kwanza katika Kundi A ikiwa na alama tatu na mabao matano ya kufunga na Uruguay inafuatia ikiwa na alama tatu na bao moja. Misri inashika nafasi ya tatu na Saudi Arabia inashika nafsi ya nne.

Goli la Jiminez linakuwa la pili katika historia ya Uruguay kupatikana katika dakika za lala salama, mwaka 1990 Daniel Fonseca alifunga bao katika dakika ya 92 katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Korea Kusini.

Uruguay inashiriki fainali za kombe la dunia kwa mara ya 13 na ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.

Misri inashiriki fainali hizi tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1990.

Ripoti ya Fredrick Nwaka

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana