Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Michezo

Hashim Thabit awanoa wachezaji wa timu ya kikapu ya Tanzania

media Hasheem Thabit akitoa mafunzo kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Kikapu TBF

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa kimataifa wa Tanzania, Hasheem Thabit amejitokeza kutoa mafunzo kwa wachezaji wa timu ya Tanzania chini ya miaka 18 inayojiandaa na michuano ya kanda ya tano Afrika.

Hashim anayechezea klabu ya Yokohama B-Corsairs aliongoza mazoezi hayo jana katika Uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yanayotazamiwa kuanza Juni 17 hadi 22 yatafanyika katika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam na kushirikisha mataifa 12.Baadhi ya mataifa hayo ni Kenya, uganda, Ethiopia, Burundi, Misri na Sudan na yatahusisha timu za wavulana na wasichana.

Wachezaji wa timu ya Tanzania ya Kikapu TBF

Akizungumza na RFI Kiswahili, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, TBF Fares Magesa maandalizi yanaenda vizuri na kwamba wahisani mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wamejitokeza kudhamini michuano hiyo.

"Tunawaomba wadau wote wa ndani na nje ya Tanzania kusaidia maandalizi ya timu yetui ya taifa na pia kuendelea kusaidia ili tufanikishe mashindano haya hapa nchini,"amesema, Magessa katika taarifa yake.

Jumla ya shilingi milioni 100 za Tanzania zinahitajika ili kufanikisha michuano hiyo na kwamba wadau wa mawasiliano wanaweza kuchangia kupitia nambari 0713/0784 6183 20 au kupitia tovuti ya shirikisho la kikapu Tanzania www.tbf.or.tz.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa michuano ya kikapu ya kanda ya tano Afrika kwa vijana chini ya miaka 18 kufanyika Tanzania.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana