Pata taarifa kuu
TANZANIA-SOKA-YANGA

Serikali ya Tanzania kusaidia mchakato wa mabadiliko, Yanga

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema itasaidia kuhakikisha klabu ya Yanga inafanikiwa katika mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Dr. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Dr. Harrison Mwakyembe The Citizen
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya serikali ya Tanzania imekuja hii leo kupitia Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe alipohudhuria mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika katika bwalo la maofisa wa Polisi, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

"Hizi timu kubwa zikitetereka zinapotea na zikipotea soka la Tanzania pia litapotea , sisi kama wizara tutahakikisha tunawatia moyo wanapofanya mabadiliko na ili wasiyumbe kwa sababu tunaamini Yanga wana kila sababu ya kwenda mbele,"amesema kiongozi huyo.

Mbali na hilo, pia klabu hiyo imepitisha bodi ya wadhamini itakayosimamia mchakato huo.

Bodi hiyo inaundwa na wajumbe wenye ushawishi mkubwa. Wajumbe wa bodi ya wadhamini waliothibitishwa leo ni Mama Fatuma Karume, George Mkuchika, Jaji Mstaafu Mkwawa, Jabir Katundu na Francis Kifukwe.

Tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wake Yusuph Manji, Yanga imekuwa ikipitia majaribu ya ndani na nje ya uwanja na kupelekea kushindwa kuetetea taji la ligi kuu msimu uliomalizika.

Yanga iliasisiwa mwaka 1935 na ni klabu yenye mafaniko makubwa  katika soka la Tanzania, ikiwa imeshinda mataji 27 ya Ligi Kuu ya nchi hiyo, ikifutiwa na wapinzani wao wakubwa Simba walioshinda mataji 19.

Ripoti ya Mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.