Pata taarifa kuu
MAN CITY-TOURE-GUARDIOLA-SOKA

Yaya Toure: Pep Guardiola mara nyingi huwa na matatizo na Waafrika

Mchezaji nyota wa Cote d' Ivoire Yaya toure amemshtumu Meneja wa Manchester City Pep Guardiola kwamba "mara nyingi ana matatizo na Waafrika, na hivyo kumchukulia kama hasimu wake.

Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure akiwa mazoezini na timu yake, ametakiwa kumuomba radhi kocha wake, Pep Guardiola.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure akiwa mazoezini na timu yake, ametakiwa kumuomba radhi kocha wake, Pep Guardiola. Reuters / Carl Recine Livepic
Matangazo ya kibiashara

“Meneja wa Manchester City Pep Guardiola "mara nyingi ana matatizo na Waafrika," kiungo wa zamani wa Blues Yaya Toure amesema.

"Sijui kwa nini lakini ninahisi kuwa alikuwa na wivu, alinuchukulia kama hasimu wake, utadhani kana kwamba kuna kitu kibaya nilichomfanyia," amesema Toure.

Yaya Toure, ambaye aliondoka katika klabu ya MAn City mnamo mwezi Mei baada ya kuichezea miaka nane, anasema anataka "kuvunja ukimya" kuhusu Guardiola, ambaye anamuelezea kuwa ni mtu mwenye "wivu".

"Labda Waafrika hawahudumiwi kama wengine," Toure amesema katika mahojiano na France Football.

Klabu ya Man City, bingwa wa Ligi Kuu imekataa kuzungumza chochote kuhusu maoni ya Toure.

Kabla ya kuondoka kwake, klabu hiyo iitwaye Yaya Touré ni moja ya misingi yake ya mafunzo na ilifunua mosai yake katika mafunzo yake.

Yaya Toure, mchezaji wa kimataifa wa Cote d' Ivoire, aliichezea Barcelona wakati ilipokua ikinolewa na Guardiola kwa misimu miwili mpaka alipouzwa kwa Man City mwaka 2010 kwa Dola Milioni 32.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.