Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA 2018-UJERUMANI

Ujerumani yatangaza kikosi chake kuelekea Kombe la Dunia

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ujerumani wametangaza kikosi cha wachezaji 23 wa mwisho watakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi mwezi huu.

Mario Gotze ameachwa kwenye kikosi cha Ujerumani, kitakachoshiriki fainali zijazo za kombe la dunia
Mario Gotze ameachwa kwenye kikosi cha Ujerumani, kitakachoshiriki fainali zijazo za kombe la dunia REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Katika kikosi hicho kocha, Joachim Law amemuacha kiungo wa Manchester City Leroy Sane ambaye aling’ara sana msimu uliopita na klabu yake ya Manchester City.

Mchezaji mwingine aliyeachwa kwenye kikosi hicho ni Mario Gotze ambaye alifunga bao la ushindi katika fainali dhidi ya Argentina mwaka 2014, mashindano yaliyofanyika nchini Brazil.

Mario Gomez amejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho baada ya kukosa fainali zilizopita nchini Brazil.

Wachezaji wengine waliojumuishwa ni pamoja na Mesut Ozil, Marco Reus, Jerome Boateng, Toni Croos, Julien Draxler na golikipa Manuel Neur ambaye kwa muda mrefu msimu huu alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha.

Wakati huo huo kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez amesema amefanya uamuzi mgumu wa kumuacha mshambuliaji wake Chrsitian Benteke katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23.

Hata hivyo, Martinez amemjumuisha beki Vicent Company ambaye aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ureno na amesema ataamua hatima ya mchezaji huyo kabla ya mechi ya kwanza dhidi ya Panama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.