Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Kiungo wa Taifa Stars asajiliwa na Petrojet FC ya Misri

media Himid Mao akiwa makao makuu ya klabu yake mpya ya Petrojet Himid Mao/Twitter

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Petrojet FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri.

Ripoti zinasema mchezaji huyo aliyekulia na kuichezea klabu ya Azam ya Tanzania kwa zaidi ya misimu saba amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo ya Misri.

Klabu yake ya Azam kupitia ukurasa wake wa Instagram kumtakia kila la kheri Himid Mao ambaye pia ni kiungo wa ulinzi katika timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Himid Mao alijiunga na Azam akiwa kidato cha kwanza na alikuwemo katika kikosi cha timu hiyo kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 2013 na pia kilitwaa ubingwa wa michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 2015.

Himid anaongeza idadi ya wachezaji wa Tanzania wanaocheza nje, wengine ni Abdi Banda anayecheza Baroka FC ya Afrika Kusini, Thomas Ulimwengu anayeitumikia Al Hilal ya Sudan, Simon Msuva anachezea Difaa Al Jadida ya Morocco, Farid Mussa wa Tenerife ya Hispania na Mbwana Samatta ambaye anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana