Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Michuano ya kuwania taji la SportPesa kupigwa Jumapili

media Klabu ya kenya ya Gor Mahia, moja ya klavu zitakazo shiriki mihuano hiyo. gormahiafc.co.ke

Awamu ya pili ya michuano ya soka kuwania taji la kampuni ya kubashiri michezo SportPesa kati ya klabu kutoka Kenya na Tanzania itaanza siku ya Jumapili katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Mshindi atapata nafasi ya kusafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na klabu ya Everton mwezi Julai.

Klabu kutoka Kenya zitakazocheza katika michuano hiyo itakayomalizika tarehe 10 ni pamoja na Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz.

Wawakilishi kutoka Tanzania ni pamoja na Young Africans, Simba SC, Singida United na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Timu hizi zote hizi zinafadhiliwa na kampuni ya SportPesa ambayo imetoa Dola 30,000 kwa mshindi huku mshindi wa pili akipata Dola 10,000.

Ratiba kamili:-

Juni 3 2018

Kakamega Homeboyz vs Yanga

Gor Mahia vs JKU

Juni 4 2018

Kariobangi Sharks vs Simba

Juni 5 2018

AFC Leopards vs Singida United

Michuano ya hatua ya nusu fainali itachezwa tarehe 7 mwezi Juni kuelekea fainali tarehe 10.

Awamu ya kwanza ya michuano hii ilichezwa mwaka 2017 jijini Dar es salaam nchini Tanzania, na Gor Mahia ya Kenya ikaibuka mabingwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana