Pata taarifa kuu
MISRI-URUGUAY-SOKA-MICHEZO

Salah: Nina imani kuwa nitacheza katika mechi dhidi ya Uruguay

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, na mchezaji wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah amesema ana amini, kuwa atakuwa amepata nafuu kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia tarehe 24 mwezi Juni nchini Urusi.

Mohamed Salah alilazimika kuondoka katika uwanja baada ya kupata jeraha mwanzoni mwa mechi.
Mohamed Salah alilazimika kuondoka katika uwanja baada ya kupata jeraha mwanzoni mwa mechi. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Salah alipata jeraha la bega mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati klabu yake ilipokuwa inamenyana na Real Madrid katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

“Upendo wenu na uugwaji mkono, utanipa nguvu,” amesema Salah.

Misri itaanza kampeni yake ya kutafuta ubingwa wa kombe la dunia dhidi ya Uruguay.

Salah, anatarajiwa kuisaidia timu yake ya taifa wakati huu akiwa na rekodi ya kuifungia klabu yake mabao 44 msimu uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.