Pata taarifa kuu
DRC-NIGERIA-EBOLA-MICHEZO

Ebola: Mechi kati ya Nigeria na DRC kuchezwa Jumatatu

Mechi ya kirafiki kati ya Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapigwa Jumatatu ya wiki ijayo licha ya mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola ulioua watu 26 nchini DRC, Waziri wa Michezo wa Nigeria, Solomon Dalung, amesema.

Timu ya taifa ya DRC "Leopards" wakati wa michuano ya AFCON 2017.
Timu ya taifa ya DRC "Leopards" wakati wa michuano ya AFCON 2017. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Super Eagles watawakaribisha nyumbani Leopards kutoka DRC katika mji wa pwani ya Port Harcourt, katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia, ambayo itaaanza mnamo mwezi Juni nchini Urusi.

"Nigeria itacheza mechi ya kirafiki na DRC," waziri amewaambia waandishi wa habari baada ya mahojiano na Rais Muhammadu Buhari mjini Abuja.

Lakini "hatua kali" zitachukuliwa, ameongeza Solomon Dalung.

"Timu itakuja kwa ndege maalum na wachezaji watafanyiwa vipimo wakati wa kuondoka kwao DRC na watafanyiwa vipimo vingine watakapowasili nchini Nigeria," amesema waziri huyo.

Serikali ya DRC na shirika la Afya Dunia (WHO), siku ya Jumatatu wiki hii, walianza kampeni ya chanjo ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo hatari katika mji wa Mbandaka, kaskazini magharibi mwa nchi, ili kuzuia janga hili.

Mwaka 2014, watu saba walifariki dunia nchini Nigeria kutokana na maambukizi ya virusi vya Ebola, wakati ambapo mlipuko wa Ebola uliokua ukiripitiwa katika baadhi ya nchi za Afrika Magharibi uliua watu 11,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.