Pata taarifa kuu
FIFA-URENO-HISPANIA

Kundi B, ni upinzani baina ya Ureno, Hispania na Morocco

Kundi B upinzani mkali unatajwa kuwa baina ya Ureno na Hispania ambayo ilishinda taji hilo mwaka 2010 nchini Afrika kusini.

Mshambuliaji wa Rela madrid, Christiano ronaldo anatazamiwa kuibeba Ureno katika fainali za mwaka huu nchini Urusi
Mshambuliaji wa Rela madrid, Christiano ronaldo anatazamiwa kuibeba Ureno katika fainali za mwaka huu nchini Urusi REUTERS/Sergio Perez
Matangazo ya kibiashara

KUNDI B

Kundi hilo lina timu za Ureno, Hispania, Morocco na Iran.

Ureno

Ureno imeshiriki fainali za Kombe la dunia mara nane. Mara ya kwanza ikiwa 1966 nchini England na mara ya mwisho ni mwaka 2014 nchini Brazil ambapo iliishia hatua ya makundi.

Fernando Santos ndiye meneja wa timu hito tangu mwaka 2014 na mafanikio yake makubwa ni kushinda taji la Euro mwaka 2016 nchini Ufaransa.

Oktoba 2017, Ureno iliifunga Uswisi mabao 2-0 na kufuzu kucheza fainali hizo, mabao yaliyofungwa na Andre Silva.

Christiano Ronaldo ndiye mchezaji bora wa Ureno na klabu yake ya Real Madrid akiwa mfungaji wa muda wote. Ni mchezaji bora wa Fifaa miaka miwili mfululizo.

Hispania

Inakwenda katikaa fainali hizi ikiwa inashika nafasi ya nane kwa ubora duniani.

Imeshiriki fainali hizo mara 16 ikiwemo ubingwa ambao walitwaa mwaka 2010.

Kipa wa zamani wa Barcelona na Real Madrid Lopetegui aliteuliwa kuchukua nafasi ya Vicente Del Bosque baada ya fainali za Ulaya za mwaka 2016.

Sergio Ramos ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi katika kikosi cha Hispania, nyuma ya Ilker Cassilas, amecheza mechi 167.

Pia Ramos alikuwemo katika kikosi cha Hispaniaa kilichoshinda fainali za Euro mwaka 2008 na 2012 na Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.

Morocco.

Inashika nafasi ya 42 kwa ubora wa viwango vya Fifa duniani.

Imeshiriki kombe la dunia mara nne na mafanikio makubwa ni kucheza hatua ya 16 bora katika fainali za mwaka 1986.

Herve Renard, kocha raaia wa Ufaransa aliyeshinda mataji mawili ya Afrika akiwa na Zambia na Ivory Coast ataiongoza Morocco katika fainali hizo. Mara ya mwisho Morocco ilicheza fainali za 1998 zilizofanyika Ufaransa.

Novemva, 11 mwaka 2017 Morocco ilijikatia tiketi ya kushiriki fainali hizo baada ya kuirarua Ivory Coast kwa mabao 2-0.

Mchezaji wa kutegemewa wa Morocco katikaa fainali hizo ni Mlinzi Mehdi Benatia, anayechezea Juventus ya Italia.

Iran

Ilikuwa timu ya tatu kufuzu kucheza fainali hizo baada ya wenyeji Urusi na wenyeji wa fainali za mwaka 2014, Brazil.

Imeshiriki fainali za Kombe la dunia mara nne, mara ya mwisho ilikuwa nchini Brazil mwaka 2014.

Inanolewa na mkufunzi mwenye uzoefu mkubwa Carlos Queroz ambaye amewahi kuifundisha Manchester United, Ureno na Afrika Kusini.

Juni 12, 2017 Iran ilifuzu kwa fainali hizo baada ya kuizamisha Urzbeijan mabao 2-0. Mehdi Terami alifunga bao moja katika mcheo huo.

Ali Daei ndiye mchezaji nyota katika kikosi cha Iran, anaichezea Rubin Kazan ya Urusi.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.