Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Mashariki ya DRC: Watu 3 wauawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama
 • Uturuki yalaani "vikali" shambulio dhidi ya msafara wa majeshi yake nchini Syria (wizara)
Michezo

Argentina, Croatia na Nigeria hapatoshi Kundi D, fainali za Kombe la Dunia

media Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi na Golikipa wa Nigeria Vincent Enyeama wakiwa uwanjani. Pedro Ugarte/AFP

Argentina, Croatia, Iceland na Nigeria zitaumana katika Kundi D, linalotajwa kuwa litakuwa na mchuano mkali.

Argentina

Ni mabingwa wa fainali za mwaka 1978 na 1986 na pia walifika fainali mwaka 2014 nchini Brazil na kupoteza kwa Ujerumani. Argentina imeshiriki fainali hizo mara 16 na kufika hatua ya nusu fainali mara tano na fainali mara tano.

George Sampaoli atakiongoza kikosi hicho maarufu kama La Alibiceleste’s katika fainali za mwaka huu.

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ecuador Oktoba 10, mwaka jana, mabao yaliyofungwa na Lionel Messi yaliiwezesha Argentina kufuzu fainali hizo licha ya kukabiliwa na kampeni ngumu.

Mchezaji nyota wa Argentina katika fainali hizo ni Lionel Messi, anatajwa kuwa miongoni mwa nyota mahiri katika mchezo wa soka duniani. Fainali za Urusi zitakuwa za nne kwa Messi tangu alipoanza kucheza michuano hiyo mwaka 2006.

Iceland

Inashiriki kwa mara ya kwanza fainali za kombe la Dunia

Heimir Hallgrimsson ndiye meneja wa kikosi hicho, alikuwemo kama meneja msaidizi wa Iceland katika fainali za Euro nchini Ufaransa ambapo timu hiyo ilifika hatua ya robo fainali.

Gylfi Sigurdsson ndiye mchezaji nyota katika kikosi cha Iceland, alifunga mabao muhimu na kusaidia upatikanaji wa mabao mengine katika mchaakato wa kufuzu fainali hizo.

Croatia

Ni mojawapo yaa mataifa madogo barani ulaya lakini imeshiriki fainali hizo mara nne. Mafanikio yao makubwa ni kushika nafasi ya tatu katika faainaali zilizofanyika nchini Ufaransa, 1998.

Zlatko Dalic ataiongoza Croatia katika fainali hizzo baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa mwaka 2017 kutoka kwa Ante Cacic.

Croatia ilifuzu fainali hizo baada ya kuitandika Ugiriki mabao 4-1 katika mechi ya mtoano. Nikola Kalinic alikuwa miongoni mwa wafungaji katika mchezo huo.

Luka Modric anayechezea Real Madrid ndio mchezaji nyota katika kikosi cha Croatia. Mchezaji huyo amejumuishwa kwenye kikosi bora cha Fifa kwa miaka mitatu mfululizo.

Nigeria

Taifa hilo la Afrika Magharibi limeshiriki fainali hizo mara tano na mafanikio makubwa ni kucheza hatua ya 16 mwaka 1994, 1998 na 2014.

Gernot Rohr raia wa Ujerumani atakiongoza kikosi cha Super Eagles akiwa na uzoefu wa kufundisha mataifa mbalimbali ikiwemo Gabon, Niger na Burkinafaso.

Oktoba 7, 2017 Nigeria ilifuzu kucheza fainali hizo baada ya kuishinda Zambia kwa bao 1-0 lililofungwa na Alex Iwobi.

John Obi Mikel ni mchezaji nyota kwenye kikosi cha Nigeria hasa katika safu ya ulinzi.

 

 

 

 

 

 

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana