Pata taarifa kuu
CAMEROON-UFARANSA-SOKA

Karl Toko Ekambi ashinda Tuzo ya Marc-Vivien Foe

Karl Toko Ekambi mchezaji wa Cameroon ameshinda Tuzo ya Marc-Vivien Foe mwaka 2018. Amepata ushindi huo Jumatatu hii Mei 14. Ekambi, mshambuliaji wa klabu ya Angers SCO amemshinda Wahbi Khazri na Bertrand Traore, katika uchaguzi wa mchezaji bora wa soka kutoka Afrika katika michuano ya Ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Mchezaji wa Cameroon Karl Toko Ekambi, mshindi wa Tuzo ya Marc-Vivien Foé 2018.
Mchezaji wa Cameroon Karl Toko Ekambi, mshindi wa Tuzo ya Marc-Vivien Foé 2018. JEAN-FRANCOIS MONIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Karl Toko Ekambi amepata pointi 264 na hivyo kushinda tuzo la MArc-Vivien Foe linalotolewa kila mwaka.

Wataalam 68 katika masuala ya soka ndio walisimamia zoezi hilo na kumtangaza Karl Toko Ekambi mshindi katika kinyang'anyiro hicho.

Ni mchezaji wa kwanza wa Cameroon kushinda tuzo hii iliyoamzishwa mwaka 2009 na ambayo ina jina la Marc-Vivien Foe tangu mwaka 2011.

Karl Toko Ekambi ameshinda uchaguzi huo, kufuatia kura iliyoendeshwa Aprili 09 hadi 26 na Radio France Internationale (RFI) pamoja na France 24. Alimshinda kwa kiasi kikubwa mchezaji wa klabu ya Tunisia ya Stade Rennes, Wahbi Khazri, (aliyepata pointi 165 na mchezaji wa Burkina FAso anayeichezea klabu ya Olympique lyonnais Bertrand Traore (pointi 61).Mchezaji wa DRC Gael Kakuta (anayeichezea klabu ya Amiens, pointi 38) na mchezaji wa mwingine wa Cameroon, Andre-Frank Zambo Anguissa (anayeichezea Olympique de Marseille, pointi 24) walishiriki kinyang'anyiro hicho.

Kwa mabao 17 katika mechi 36, Karl Toko Ekambi, mzaliwa wa Paris amechangia kuiimarishaklabu ya Angers SCO katika daraja la kwanza.

Wachezaji walioshinda Tuzo ya Marc-Vivien Foe

2009*: Marouane Chamakh (Bordeaux/Morocco)
2010*: Gervinho (Lille/Côte d'Ivoire)
2011: Gervinho (Lille/Côte d'Ivoire)
2012: Younès Belhanda (Montpellier/Morocco)
2013: Pierre-Emerick Aubameyang (Saint-Etienne/Gabon)
2014: Vincent Enyeama (Lille/Nigeria)
2015: André Ayew (Marseille/Ghana)
2016: Sofiane Boufal (Lille/Maroc)
2017: Jean Mickaël Seri (Nice/Côte d’Ivoire)
2018: Karl Toko Ekambi (Angers SCO/Cameroon)
* Ilikua bado haijaitwa Tuzo ya Marc-Vivien Foé.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.