Pata taarifa kuu
KENYA-URUSI-OLIMPIKI-MICHEZO

Asbel Kiprop: Sijawahi kutumia dawa aina ya EPO

Mwanariadha kutoka nchini Kenya Asbel Kiprop, bingwa wa mbio za Mita 1500 katika Mashindano ya dunia na Olimpiki amekuwa na wakati mgumu katika siku za hivi karibuni baada ya ripoti kuwa amekuwa akitumia dawa zilizopigwa marufuku ili kumsaidia kupata ushindi katika mashindano mbalimbali.

Bingwa wa Mashindano ya Olimpiki Asbel Kiprop anadai kuwa amekuwa na msongo wa mawazo baada ya Gazeti la Uingereza Daily Mail kuripoti kuwa anatumia madawa ya kusisimua mwili.
Bingwa wa Mashindano ya Olimpiki Asbel Kiprop anadai kuwa amekuwa na msongo wa mawazo baada ya Gazeti la Uingereza Daily Mail kuripoti kuwa anatumia madawa ya kusisimua mwili. twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Wakati uchunguzi ukiendelea kuthibitisha hilo, Kiprop mwenye umri wa miaka 28 ameendelea kukanusha kuwahi kutumia dawa aina ya EPO kama inavyodaiwa ili kumwongezea nguvu mwilini.

Bingwa huyo wa michezo ya Olimpiki mwaka 2008 jijini Beijing nchini China, na michezo ya dunia mwaka 2011 mjini Daegu, Korea Kusini, Moscow, Urusi mwaka 2013 lakini pia Beijing mwaka 2015, amekuwa na msongo wa mawazo baada ya Gazeti la Uingereza Daily Mail kuripoti madai haya.

Historia inaonesha kuwa, matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini kwa wanamichezo, ni jambo ambalo lilianza zamani sana wakati michezo ya Olimpiki ya kwanza ilipoanza kati ya mwaka wa 776 hadi 393, kabla ya Kristo.

Wanamichezo wanaoshiriki katika michezo hasa riadha, kukimbiza Baiskeli, bondia, baseball hata soka ni miongoni mwa michezo ambayo dawa hizi zinaendelea kutumiwa, hasa wakati wa mashindan makubwa.

Mwaka 1904 mwanariadha kutoka Marekani Thomas Hicks, alitumia mchanganyiko wa heroin na cocaine, uliomsaidia kushinda mbio za Marathon kwa upande wa wanaume wakati wa michezo ya Olimpiki , iliyofanyika Marekani. Licha ya kushinda mbio hizo, karibu apoteze maisha kutokana na matumizi hayo.

Mambo yalikuwa mabaya mwaka 1967, baada ya mkimbiza baiskeli raia wa Uingereza Tommy Simpson, kupoteza maisha baada ya kufika katika hatua ya 13 ya mashindano ya kwanza ya Tour de France.

Baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa alitumia kiasi kikubwa cha dawa inayofahamika kama amphetamines na kumsababisha shida katika mwili wake.

Kufikia hatua, Mashirika mbalimbali ya michezo yalianza kufikia namna ya kukabiliana na tatizo hili ambalo lilikuwa linaendelea kuwa kubwa katika medani ya michezo mbalimbali.

Baadaye mwaka huo, Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki iliunda Tume ya kupambana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku, kwa lengo la kuwalinda wanamichezo na kuweka usawa katika ushindani wa michezo mbalimbali.

Vipimo vya kwanza, kubaini iwapo wachezaji wametumia dawa zilizopigwa marufuku, vilifanyika mwezi Februaru mwaka 1968 wakati wa Michezo ya Olimpiki katika mji wa Mexico City.

Miongoni mwa matukio ya kihistoria jkatika vita dhidi ya matumizi ya dawa hizi ilikiuwa ni Septemba 27 mwaka 1988 wakati wa Michezo ya Olinpiki jijini Seoul nchini Korea Kusini, mwanariadha kutoka Canada Ben Johnson, aliyekuwa anakimbia mbio fupi kupokonywa medali ya dhahabu baada ya kubainika kuwa alitumia dawa za kumwongezea dawa mwilini, na mwaka 1993 akafungiwa maisha.

Mbali na kuwasaidia wachezaji kushinda, kuna baadhi ya wanamichezo ambao walipoteza maisha kama mchezaji wa soka wa Marekani Lyle Alzado aliyepoteza maisha, baada ya kutumia dawa aina ya Steroids na HGH, alizotumia kwa muda mrefu.

Mwaka 1999, kulikuwa na kongamano la michezo walikutana jijini Lausanne nchini Uswizi na kuamua kuunda taasisi ya dunia itakayokuwa inapambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa wanamichezo WADA.

Miongoni mwa wachezaji waliowahi kufungiwa na Kamati ya Kimataifa ya Michezo IOC, baada ya uchunguzi wa WADA ni pamoja Mwanariadha Mmarekani Marion Jones ambaye baada ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2000, alipokonywa medali ya dhahabu katika mbio za Mita 100 jijini Sydney nchini Australia.

Martina Hingis kutoka Uswizi, bingwa zamani wa mchezo wa Tennis na nambari moja duniani,alipatikana kutumia dawa ya kulevya aina ya Cocaine. Mchezaji mwenzake Richard Gasquet raia wa Ufaransa amewahi pia kupatikana na matumizi ya Cocaine.

Mwaka 2011, Shirikisho la soka duniani FIFA, lilitangaza kuafungua wachezaji watano wa Korea Kaskzini amabo walbainika kutumia dawa aina ya steroids wakati wa michuano ya kombe la dunia.

Mwaka 2012, Lance Armstrong aliyekuwa bingwa mara saba wa mashindano ya kukimbiza Baiskeli ya Tour de France, alipokonywa mataji hayo yote baada ya kubainika kuwa alikuwa anatumia dawa zilizopigwa marufuku. Hatua hii ilichukuliwa na USADA, Shirika la kupambana na dawa hizi nchini Marekani, lakini Armstromg akakataa kwenda kujitetea.

Alberto Contador ni mkimbiza baiskeli mwingine, kutoka Uhispania ambaye alipokonywa taji lake la Tour de France mwaka 2010, baada ya kubainika kuwa alitumia dawa aina ya clenbuterol baada ya kula nyama wakati wa mapumziko wakayi wa michezo hiyo.

Mwaka 2016, baada ya uchunguzi wa WADA, Kamati ya Michezo ya Olimpiki, iliifungia Urusi kushiriki katika michezo ya Olimpiki mwaka huo nchini Brazil, baada ya kubainika kuwa, serikali ta Moscow ilikuwa inashiriliana na wanamichezo wake kuwapa dawa zilizopigwa marufuku kuwaongezea nguvu mwilini.

Serikali ya Urusi imeendelea kukanusha madai haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.