sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atangaza kujiuzulu
Michezo

SportPesa yarejea kufadhili soka nchini Kenya

media Mkurugenzi wa SportPesa Ronald Karauri (Kushoto), Waziri wa Michezo Rashid Achesa (Katikati) na rais wa Shirikisho la soka FKF Nick Mwendwa (Kulia) wakiwahotubia wanahabari Aprili 23 2018 twitter.com

Kampuni ya kubashiri mchezo SportPesa, imerejesha ufadhili wa ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL.

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa Ronald Karauri amesema kampuni yake itatoa Shilingi Milioni 685 kufadhili soka nchini humo kwa muda wa miaka mitatu ijayo.

Kati ya fedha hizo, Shirikisho la soka FKF, itapata Shilingi Milioni 69 huku ligi kuu KPL ikipangiwa Milioni 259.

Klabu ya Gor Mahia inayoshiriki michuano ya Shirikisho, itapokea Shilingi Milioni 198 huku AFC Leopards ikinufaika na Shilingi Milioni 159.

Hata hivyo, SportPesa haitaendelea na ufadhili wa michezo ya raga na bondia kama ambavyo ilikuwa inafanya hapo awali.

Mwaka uliopita, SportPesa ilijiondoa katika ufadhili wa michezo nchini humo baada ya serikali kuitaka kulipa kodi ya asilimia 35 kutoka kwa mapato inayokusanya kila mwaka.

Hii hatua kubwa kwa maendeleo ya mchezo wa soka nchini humo hasa kwa klabu ya Gor Mahia na AFC Leaoprds ambazo zina historia ndefu ya soka nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana