Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Yanga, Gor Mahia na Rayon Sports kuwania taji la Shirikisho la soka Afrika

media Kikosi cha wachezaji wa Gor Mahia. gormahiafc.co.ke

Vlabu tano kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati vimefuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho la soka barani Afrika baada ya michuano ya mwondoano kumalizika siku ya Alhamisi.

Vlabu vilivyofuzu baada ya kupata matokeo mazuri ni Al Hilal ya Sudan, AS Vita Club ya DRC, Yanga ya Tanzania, Gor Mahia ya Kenya na Rayon Sports ya Rwanda.

Licha ya kufungwa bao 1-0 na Welayta Dicha ya Ethiopia, ushindi wa Yanga wa mabao 2-0 nyumbani uliwasaidia kufuzu katika hatua hiyo.

Nayo Gor Mahia ya Kenya ambayo imeweka historia kwa kufuzu katka hatua hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya miaka 31 iliposhinda taji la Afrika, licha ya kufungwa na SuperSport United mabao 2-1 ugenini, ushindi wao wa bao 1-0 uliwasaidia.

Mambo yalikuwa mazuri pia kwa Rayon Sport ya Rwanda ambayo licha ya kupoteza kwa mabao 2-0 baada ya kufungwa na Costa do Sol ya Msumbiji, ushindi wake wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ulitosha kuwasaidia.

Vlabu 16 zimefuzu katika hatua ya makundi, na sasa droo itafanyika siku ya Jumamosi ambapo kutakuwa na makundi manne, kila kundi na vilabu vinne.

Orodha ya vlabu vilivyofuzu:-

USM Alger (Algeria)

Al Hilal (Sudan)

AS Vita Club (DRC)

Enyimba (Nigeria)

ASEC Mimosas (Cote Dvoire)

Young Africans (Tanzania)

CARA Brazavulle (Congo)

Williamsville AC (Cote Dvoire)

Al-Masry (Misri)

Aduana Stars (Ghana)

Gor Mahia (Kenya)

Djoliba (Mali)

Raja Casablanca (Morocco)

RS Berkane (Morocco)

UD Songo (Msumbiji)

Rayon Sport (Rwanda)

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana